Kakuma Green Solutions, timu ya vijana wakimbizi kutoka Kambi ya Kakuma, imeshinda nafasi ya kwanza na zawadi ya €1,000 katika mashindano ya Social Impact Award ya Afrika Mashariki 2026, yanayoandaliwa na Social Innovation Academy (SINA).
Timu hiyo inatumia kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi (climate-smart agriculture) kulima mboga ndani ya jamii ya wakimbizi, ikishirikiana na wajasiriamali wanawake wanaouza mboga hizo kwa familia za kambini.
Kwa ushindi huo, timu hiyo itasafiri hadi Podgorica, Montenegro, kuhudhuria mkutano wa Social Impact Award Summit utakaofanyika tarehe 24–27 Novemba 2026.
Ushindi huu ni ushahidi mwingine kwamba Kakuma ni nyumbani kwa vipaji na wabunifu, si mahali pa kukata tamaa.
*Chanzo: Social Innovation Academy —

