Walimu wakimbizi katika kambi za Dadaab na Kakuma wanadai kutambuliwa kitaaluma, mishahara bora na fursa sawa za kujiendeleza kama walimu wa Kenya, wakisema mchango wao katika kuelimisha watoto wakimbizi unastahili heshima na msaada zaidi.
Wakizungumza na Shirika la Save the Children Kenya kupitia mradi wa TeachWell Voices, walimu hao wameeleza changamoto za kufanya kazi bila usajili wa Tume ya Huduma za Walimu (TSC), pamoja na kukosa fursa zinazopatikana kwa wenzao wa Kenya.
Leila, mwalimu mkimbizi wa Dadaab, amesema utambulisho ndilo tatizo kubwa: "Most refugee teachers are not recognised. They do not have the TSC number." Ameongeza kuwa anatumai walimu wakimbizi watatambuliwa na TSC ili wapate mipango, mishahara na malengo sawa na walimu wa taifa.
Yusuf, mwalimu mwingine wa Dadaab anayeishi kambini tangu mwaka 1992, amesema: "Refugee teachers, we normally take little pay compared to the Kenya national teachers."
Kwa mujibu wa Save the Children, walimu wakimbizi ni zaidi ya asilimia 80 ya walimu wote katika shule za kambini, lakini wengi wao hulipwa takriban KSh 8,000 kwa mwezi, ikilinganishwa na KSh 22,800 kwa walimu wa Kenya — na baadhi ya madarasa hufikia uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 96.
Viongozi wa shule wamesema shule za kambini zinawategemea sana walimu wakimbizi, na wanatoa wito wa kuingizwa rasmi katika mfumo wa elimu wa Kenya.

