Canada imezindua rasmi leo, Alhamisi Novemba 12, 2026, mradi wa STEP (Strengthening Skills Training Ecosystems and Pathways) — mradi wa miaka saba wa mafunzo ya ujuzi na ajira kwa vijana 10,000 wa Dadaab, Kakuma na Kalobeyei.
Uzinduzi ulifanyika katika Ban Ki-moon Hall, ndani ya UNHCR compound, Dadaab. Mradi huu ulitangazwa Novemba 10 — leo umezinduliwa rasmi, na hii ni hatua ya pili, si tangazo lile lile.
Mradi unafadhiliwa na Global Affairs Canada na unatekelezwa na World University Service of Canada (WUSC), na utaendeshwa kuanzia 2026 hadi 2033. Kulingana na Kenya News Agency, mradi huu una thamani ya KSh 1.65 bilioni.
Watakaofaidika ni vijana 10,000 — 60% wakimbizi na 40% jamii wenyeji (host communities) wa Dadaab, Kakuma na Kalobeyei.
Uzinduzi uliongozwa na Balozi Mkuu wa Canada nchini Kenya, Joshua Tabah. Idara ya Refugee Services (DRS) iliwakilishwa na Mercy Mwasaru, Acting Commissioner for Refugee Affairs.
Vijana watakaoshiriki watafaidika na: mafundo ya biashara na ruzuku kwa vijana 5,500; ajira za kidigitali 1,800; mafunzo ya TVET na internships 2,500; na nafasi 200 za kwenda kufanya kazi Canada na kwingine.
Tarehe na utaratibu wa kujiandikisha bado haujatajwa — tutawajulisha mara itakapotoka. Usikose kufuatilia.
Chanzo: Wajir Today — https://wajirtoday.co.ke/canada-launches-seven-year-youth-skills-project-targeting-10000-in-garissa-turkana/

