Demalo Rispa, msanii mdogo wa Kakuma, ametoa video rasmi kamili ya wimbo wake mpya "Piir ë Kakuma" akiwa na JCA. Video hiyo ilianza kuonekana jana jioni (Nov 4) na ni ya dakika 2:51 — si trailer, ni video kamili.
Hii ni habari kubwa kwa muziki wa kambi: Demalo ni mmoja wa wasanii wadogo wanaojitahidi kwa mikono yao, na channel yake ina subscribers 128 tu — lakini video hii tayari imefikia watu zaidi ya 600 kwa masaa machache. Kila view, kila share, ni kuni inayowasha moto wa msanii wa kambi.
Kama unapenda muziki wa Kakuma, huu ni wakati wa kumsikiliza Demalo na kumsaidia kufika mbali. Wimbo unapatikana kwenye YouTube.
Chanzo: Demalo Rispa Official (YouTube) — https://www.youtube.com/watch?v=gwu7LHkM4HA

