Ni Familia, Sio Uzembe! Msanii Evlo Big Star Ajitetea Juu ya Ukosoaji wa ‘Song Surgery’ na Kuahidi Video Kali Mwaka Huu.
Je, umewahi kuusikiliza wimbo wa msanii na ukapenda sana, lakini video yake ikawa chini ya kiwango?
Hili ndilo suala ambalo mchambuzi Official Abi wa kipindi cha Song Surgery cha Secret Of Future alimkosoa nalo msanii Evlo Big Star. Abi alisisitiza kuwa Evlo anatoa audio (sauti) kali sana, lakini video zake zinaiangusha sanaa ya Kakuma .
Sasa, Evlo Big Star ameketi kwenye mahojiano maalum na kufunguka kuhusu ukweli wa mambo. Hajapinga ukosoaji huo, badala yake ameufafanua kwa kina kwanini msanii huwa anapotea na kwanini pesa ndiyo huamua video gani utatoa!.
Hadithi yake ni ya kweli na inagusa hisia za kila msanii independent. Endelea kusoma ili kujua kwanini "video kali ya kimataifa" ya 'No Wow' ilimshinda kuifanya tena, na ahadi yake kuhusu ngoma ya 'Fine CC'!
Evlo Big Star Azungumzia Changamoto Tatu (3) Kuu
Evlo Big Star anaanza kwa kukubali ukweli wa maneno ya Abi , lakini anasisitiza kuwa ni rahisi kukosoa bila kuelewa 'situations' ambazo msanii anapitia. Haya ndio mambo makuu matatu aliyoyafichua:
1. Mzigo wa Familia Dhidi ya Video Kubwa
Msanii Independent: Evlo anasema yeye ni msanii anayejibeba mwenyewe, hajawahi kuwa na meneja. Hana sapoti kubwa kama wasanii wengine ambao wazazi au watu wanamchangishia.
Kipaumbele cha Pesa: Changamoto kubwa kwake ni ushindani kati ya kazi ya sanaa na majukumu ya nyumbani. Anasema: "I have family I have to handle the problems". Hii humfanya kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya familia, na pesa anazopata huishia huko, badala ya kurekodi video za kiwango cha juu.
"Pesa Yako Ndo Inaruhusu": Alitetea uamuzi wake kwa kusema: "Pesa zako ndio zinaruhusu sasa wewe yaani utatoa video gani. Sasa kusema kwamba oh hii video huyu mtu alifaa afanye hivi... Director angemcharge ngapi?". Anasisitiza kuwa kiwango cha video huendana na budget.
2. Kupotea kwa Malengo na Audios Nyingi
Hasara ya Audios: Evlo anakubali kosa alilojifunza kupitia ushauri na Song Surgery — kwamba alikuwa akitoa 'songs songs songs, audio audio audio' nyingi ambazo hazikuwa na faida kwani hazikufika mbali au kumtambulisha msanii.
Hadithi ya Kutotambuliwa: Alisimulia jinsi alivyokutana na jamaa Nairobi aliyeskia wimbo wake lakini hakujua ni nani aliimba mpaka aliposikia "Evlo Bigstar Once Again" kwenye wimbo. Hii ilimfanya aelewe kuwa kazi inahitaji kumtambulisha msanii.
3. Ahadi ya 'Sure Video' na Maono
Mwelekeo Mpya: Evlo ameahidi badala ya kutoa audios nyingi, anakuja na "sure video yenye iko na sure song".
Video ya 'Fine CC': Aliweka wazi kuwa video ya ngoma yake 'Fine CC' inakuja na alikuwa amepanga kuitoa Septemba, lakini director alikuwa busy. Anasisitiza kuwa lazima atoe video kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Ujumbe kwa Wasanii na Tuzo za Secret of Future
Tuzo na Mafanikio: Evlo aliwatakia heri wale wote walionominate kwa Tuzo za Secret of Future 2025. Hata hivyo, aliwashauri wasiilemaze (usiwalemaze) kuwazuia kuendelea na muziki, akisema tuzo isiwe sababu ya wao kusimama au kujiona wamefika.
Kauli ya Mwisho kwa Wasanii: Ujumbe wake ni mmoja: "Tufanye kazi buse kazi zetu ndio zitatupeleka mbele. Beta kazi zikutambulishe badala wewe kutambulisha kazi.".
Evlo Big Star anawashukuru sana mashabiki wake kwa upendo wao na anaomba wamupe muda kidogo ili arekebishe mambo na kuwaletea kazi yenye hadhi.
"Ni swala la muda tu... Evlo Big Star, best man in town, atakuwa hapa kuwafurahisha kila time."
Endeleeni kumpa sapoti! Tazama mahojiano haya kamili hapa: EVLO BIG STAR | PESA ZAKO NDIO ZINA RUHUSU WEWE KUTATUA VIDEO NGANI, NISAFARI NI NDEFU, FAMILIA