Skip to main content

Java Boy: Kutoka Kakuma Hadi Kwenye Ulimwengu wa Muziki!


Simba wa Kambi: Safari ya Muziki ya Java Boy Kutoka Kakuma
Karibuni wapenzi wa muziki! Leo,

Tunamwangazia msanii mahiri kutoka Burundi, anayeishi Kakuma, ambaye anatikisa tasnia ya muziki kwa upekee wake. si mwingine bali ni Java Boy, "Simba wa Kambi" mwenyewe!
Java Boy anasimulia safari yake ya muziki, akieleza jinsi alivyogundua kipaji chake na kuamua kujitosa kikamilifu.
Alianza kwa kuiga wasanii wengine, lakini baadaye akajitambua na kuanza kutengeneza muziki wake mwenyewe.
Safari yake haikuwa rahisi. Alikumbana na changamoto nyingi, ikiwemo watu waliomkatisha tamaa na gharama za studio za kurekodi . 

Lakini hakukata tamaa. Alivumilia na sasa anafurahia matunda ya kazi yake.
Java Boy ametoa nyimbo nyingi, lakini wimbo wake anaoupenda zaidi ni "Waimi," unaoelezea maisha ya wakazi wa kambini. Anafanya muziki wa Afro Bongo na Amapiano , na anaamini ana kipaji kikubwa kwa sababu kila wimbo wake unafanya vizuri.
Ana ndoto ya kufanya kolabo na wasanii wengine kama Young G na Panado. Pia, alishinda tuzo ya "Story Matter Behavior Change" katika mashindano aliyoshindana na wasanii wakongwe .

Java Boy anawashauri wasanii wenzake kuepuka majivuno, na anawaomba mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono .


Je, ungependa kujua zaidi kuhusu muziki wa Java Boy au wasanii wengine kutoka Kakuma?

tembele kwenye channel yetu ya youtube kutazama yajayo

Comments

Designed by Open Themes & Nahuatl.mx.